Lipi Lenye Faida Zaidi; Kulingania Katika Da'awah Au Kutafuta Elimu Kwanza? Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah) SWALI: Ni jambo lipi katika haya mawili ni bora? Kutafuta elimu au kulingania watu kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kwa sababu nilisikia baadhi ya makundi yakisema: "Da'wah kwa ajili ya Allaah ni yenye faida kubwa kulikoni kutafuta elimu." JIBU: Kutafuta elimu ni jambo la mwanzo kabisa, kwa sababu haiwezekani mtu kuweza kuwalingania watu katika Dini ya Allaah mpaka awe na elimu; ama akiwa hana elimu basi hawezi kuwalingania watu katika Dini ya Allaah, na ikiwa atafanya (Da'wah) basi atakayokosea yatakuwa makubwa zaidi kuliko atakayopatia. Kwa hiyo, ni sharti kwa Mlinganiaji kuwa na elimu kabla ya kuanza kulingania watu; haya ni kutokana na kauli Yake Allaah: قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَ سُبْحَانَ