Shaykh Swaalih Al-Fawzaan - Lipi Lenye Faida Zaidi; Kulingania Katika Da'awah Au Kutafuta Elimu Kwanza?
Lipi Lenye Faida Zaidi; Kulingania Katika Da'awah Au Kutafuta Elimu Kwanza?
Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)
SWALI:
Ni
jambo lipi katika haya mawili ni bora? Kutafuta elimu au kulingania
watu kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Kwa sababu nilisikia
baadhi ya makundi yakisema: "Da'wah kwa ajili ya Allaah ni yenye faida
kubwa kulikoni kutafuta elimu."
JIBU:
Kutafuta
elimu ni jambo la mwanzo kabisa, kwa sababu haiwezekani mtu kuweza
kuwalingania watu katika Dini ya Allaah mpaka awe na elimu; ama akiwa
hana elimu basi hawezi kuwalingania watu katika Dini ya Allaah, na ikiwa
atafanya (Da'wah) basi atakayokosea yatakuwa makubwa zaidi kuliko
atakayopatia. Kwa hiyo, ni sharti kwa Mlinganiaji kuwa na elimu kabla ya
kuanza kulingania watu; haya ni kutokana na kauli Yake Allaah:
قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَ سُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ
Sema:
“Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah, juu ya baswiyrah (nuru ya
elimu, ujuzi, umaizi) mimi na anayenifuata. Na Subhaana-Allaah
(Utakasifu ni wa Allaah), nami si miongoni mwa washirikina.” [Yuwsuf: 108]
Hata
hivyo; kwa mambo ya wazi (yanayojulikana na kila mmoja) Inawezekana kwa
mtu wa kawaida kulingania katika mambo hayo; kama kuamrisha Swalaah na
kukataza kuipuuza (Swalaah), kuamrisha Swalaah ya Jamaa’ah (kwa
wanaume), kuamrisha watoto kuswali; mambo haya yanafahamika kwa (wote);
mtu wa kawaida na mtafutaji elimu.
Hata
hivyo; mambo ambayo yanahitaji ufahamu na ujuzi kuhusu Halaal na Haraam
na mambo ya Shirk na Tawhiyd, hayo basi lazima kutafutwe elimu katika
hayo. Kwa ujumla, wote wanaosema ya kuwa; Kufanya Da'wah ni jambo lenye
kunufaisha kulikoni kusoma, hao ni Jamaa’at At-Tabliygh na hao ni katika
kundi potofu la uzushi la Kisufi.
Maoni