Ruka hadi kwenye maudhui makuu

FAIDA ZA KITUNGUU SWAUM

KITUNGUU THAUM (Swaumu/Saumu):

Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni kitunguu swaumu. Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa.

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum . Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.

Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu.
Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Warumi. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana. Kuna baadhi ya imani watu wanaamini kitunguu swaumu kina uwezo wa kufukuza hadi wachawi! hivyo kama unatokewa unapata usingizi wa usioeleweka au unakabwa kabwa na wachawi hebu jaribu kitunguu swaumu na utuletee mrejesho

Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash).

Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake. Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.

Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
kitunguu swaumu
Kigawanyishe katika punje punje
kitunguu swaumu
chukua punje 6
kitunguu swaumu
Menya punje moja baada ya nyingine
kitunguu swaumu
Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
kitunguu swaumu
Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.

Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea kung’aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia (bila shaka Tanga fresh watanipa hela ya soda kwa kuwapigia promo)!

Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.

Kitunguu swaumu kilichokatwakatwa/chopped
Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30
Haya ni baadhi ya magonjwa yaliyothibitika kutibika na yanatibika au kukingika na kitunguu swaumu:
1. Huondoa sumu mwilini
2. Husafisha tumbo
3. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
4. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
5. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
6. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
7. Huondoa Gesi tumboni
8. Hutibu msokoto wa tumbo
9. Hutibu Typhoid
10. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
11. Hutibu mafua na malaria
12. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
13. Hutibu kipindupindu
14. Hutibu upele
15. Huvunjavunja mawe katika figo
16. Hutibu mba kichwani
17. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
18. Huzuia meno kung’ooka na kutuliza maumivu
19. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
20. Hutibu maumivu ya kichwa
21. Hutibu kizunguzungu
22. Hutibu shinikizo la juu la damu
23. Huzuia saratani/kansa
24. Hutibu maumivu ya jongo/gout
25. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
26. Huongeza hamu ya kula
27. Huzuia damu kuganda
28. Husaidia kutibu kisukari
29. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
30. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.
Nini madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji
Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Kumbuka kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MTAMBUE JINI MAHABA NA TIBA YAKE

ASALAMU ALAYKUM M aisha ya mwanadamu yamezungukwa na misukos uko na mitihani mbalimbali ambayo wakati mwingine humfanya ajione tofauti na kujiona mwenye kukosa thamani ya maisha, miongoni mwa matatizo ambayo huyapata wengi katika ulimwengu tulionao ni tatizo la jini mahaba nalo huwa pa watu weng i fadhaiko na kukosa amani na raha ya maisha  JINI MAHABA NI NINI? J ini mahaba ni jini {pepo,shetani} yeyote alie muingia mwanaadamu kwa lengo la kufanya nae uchafu wa zinaa. VIPI ANAWEZA KUMUINGIA MTU?     J ini mahaba hu waingia watu kwa sababu nyingi m iongoni mwazo ni kulala bila ya nguo au nguo nye pesi sana bila ya kusoma dua hasa nyakati za jo to 2.wakati wa kufanya tendo la ndoa na wanandoa kusahau kusoma dua wakati wa tendo{na hapa ndipo huwaingia watu zaidi} 3.kujitazama ktk kioo kwa muda mrefu bila ya kusoma dua na hasa kwa wanaopenda kujitazama waki wa uchi 4.kuogelea ukiwa uchi katika vyanzo vya maji bila ya dua {hii hupelekea kuingiwa hasa na majini aina

TIBA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

ASALAMU ALAYKUM     katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya jiji la dar na ulimwengu kwa ujumla imekuwa ni jambo la kawaida kuona mara kwa mara uuzwaji wa zinazoitwa dawa za kuongeza nguvu za kiume            jambo ambaloz amani halikuwepo kwani watu waliweza kuwa na nguvu za kutosha kulimudu tendo la ndoa bila kuhitajia dawa yoyote ile leo imekuwa kama desturi kama hujui dawa ya nguvu za kiume wewe hutakuwa mganga na hutapata mtu wa kumtibu kwani ni zaidi ya asilimia 60% ya wtakao hitaji tiba watahitaji dawa ya nguvu za kiume jambo lililonipelekea kuandika makala hii ambayo nataraji itakuwa na manufaa kwa wengi  NGUVU ZA KIUME Ni hali ya mtu kuweza kumudu tendo la ndoa na kiasili hakuna ugonjwa wa nguvu za kiume bali kuna upungufu wa nguvu za kiume NINI CHANZO CHA TATIZO HILI kuna sababu nyingi znazopelekea upungufu wa nguvu za kiume miongoni mwazo ni; kuugua kwa muda mrefu matatizo ya ngiri .   hili ni katika janga kubwa miong

tiba ya pumu

TIBA YA KIFUA CHA PUMU Wednesday, September 14, 2016 8:19 PM Kwa wenye kusumbuliwa na pumu tafuta dawa inayoitwa lufyambo chukua majani yake kiasi cha ujao wa viganja viwili chemsha katika maji lita moja na nusu weka ndimu za maji kumi iache ichemke hadi ibakie nusu lita tumia kunywa kikombe cha kahawa kutwa mara mbili kwa muda wa wiki mbili in shaa alla utapona            Huu ndio waitwa lufyambo Kwa maswali tiba maoni na ushauri +255 652 886 693 Whatsapp +255 685 306 407 Email. Drahmash@gmail.com