Ruka hadi kwenye maudhui makuu

JINI GHAWAAS NA TIBA YAKE

Jini ghawaas na tiba yake

ghawas ni neno la kiarabu lenye maana ya mzamiaji *mpiga mbizi* mara nyingi linapotumiwa neno hili hukusudiwa anaezamia ili kutafuta madini ktk bahari km lulu n.k
kama vile ilivyokuwa kwa nabii suleymaan a.s
ktk sura ya 38 allah
anasemaوَالشَّيَاطِينَ كُلَّ بَنَّاءٍ وَغَوَّاص
ٍ

Na tukayafanya mashet'ani yamtumikie, wote wajenzi na wapiga mbizi.
wakikusudiwa majinu waliokuwa wakifanya kazi ya kuzamia baharini kutafuta lulu na madini mengine baharini

majini hawa wameitwa ghawas kwa sababu ya kuishi kwao ktk vyanzo vya maji na kupendelea sana maeneo yenye majimaji

vipi humuingia mwanadamu

jinu huyu humuingia mtu mara nyingi kwa kutumwa na wachawi  au kuchokozwa hasa kwa wale wenye kuogolea bila kupiga bismilahi kupiga makelele ktk vyanzo vya maji km kisimani bwawani baharin ziwan kujisaidia ktk vyanzo ya maji kujamiiana ktk vyanzo vya maji vichochoroni na maporini kuoga bila ya nguo ktk mito bahari ziwa au mabwawa n.k ambapo ndio makazi yao

*Wenyeji wa kigoma ujiji wanafahamu uwepo wa chemchem ya rutale *mwami ntale* *iliyopo kando ya ziwa tanganyika ambayo humwaga maji yake ktk ziwa hilo*

*chemchem hii ni ktk maeneo ambayo majini wanaishi na wakazi wa ujiji* *kazaroho na maeneo ya jirani wana historia kubwa ya matukio ya ajabu kutokea ktk chemchem hii hasa majira ya mchana jua* *likiwa kali au kukiwa na kelele hushuhudiwa maji yakitibuka na kuwa mekundu ama kuonekanwa nyoka* *wakicheza ktk maji*
*kwa sasa eneo hilo limewekewa uzio ili watu wasifike ktk chanzo cha hio chemchem*

ukiachana na hilo pia kwa wavuvi na wazamiaji ni jambo la kawaida kuona viumbe hawa ktk maji na huweza kuona km watu wapo ktk nyumba na wakiishi bila tatizo hawa ni ktk majini aina ya ghawaas ambao huko ndio maskani mwao

DALILI ZAKE
Alie sibiwa na aina hii ya majini huwa na dalili hizi
1. kupenda sana kuchezea maji na kuogelea na ikiwa hawezi kuogelea hupenda kwenda ktk vyanzo vya maji aangalie tu mandhar yake
2. ndoto za kuota viumbe wa baharini km samaki n.k
kuota samaki mara kwa mara ama kuota samaki km sio mara kwa mara humaanisha mali kulingana na namna ya uotaji wake
3. kupenda kuoga maji baridi hata ikiwa kuna baridi kali
4. mgonjwa hupenda sana kwenda chooni hata kama hana haja
4. kupiga makelele na kukimbia ovyo
5. kutoka uvimbe usio na maumivu kisha hupotea na baada yabmuda hutokea tena aghalabu huwa una hama hama
*ahmashherbal.blogspot.com*
6. kuwashwa mwili
7. kuhisi kama unatambaliwa na wadudu na ukijipangusa huwaoni
8. kutoka vipele au vidoadoa vyekundu mwilini
9. mipango kuharibika bila sababu za msingi

TIBA YAKE
asomewe ruqya siku 14 mfululizo
atumie dawa hizi
miatu saila kibiriti upele chumvi ndimu ya unga na bua la mtama la miaka miwili au zaidi
changanya pamoja na bua utaliponda ponda uchanganye na hizo dawa
utajifukiza asubuhi na jioni siku 14

chukua usembe bahari kizabuni na lukuta
changanya kiasi sawa utatumia kuoga asubuhi na jioni siku 14

msaka uchawi mkunazi sokondi kizabuni mwavi
ziwe kiasi sawa utatumia kunywa ktk uji mwepesi kijiko kimoja cha dawa ktk uji kikombe kimoja asubuhi na jioni siku 14

kwa maswali maoni ushauri na tiba wasiliana nasi
whatsapp& call
+255 685 306 407
+255 652 886 693
email:drahmash@gmail.com

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

MTAMBUE JINI MAHABA NA TIBA YAKE

ASALAMU ALAYKUM M aisha ya mwanadamu yamezungukwa na misukos uko na mitihani mbalimbali ambayo wakati mwingine humfanya ajione tofauti na kujiona mwenye kukosa thamani ya maisha, miongoni mwa matatizo ambayo huyapata wengi katika ulimwengu tulionao ni tatizo la jini mahaba nalo huwa pa watu weng i fadhaiko na kukosa amani na raha ya maisha  JINI MAHABA NI NINI? J ini mahaba ni jini {pepo,shetani} yeyote alie muingia mwanaadamu kwa lengo la kufanya nae uchafu wa zinaa. VIPI ANAWEZA KUMUINGIA MTU?     J ini mahaba hu waingia watu kwa sababu nyingi m iongoni mwazo ni kulala bila ya nguo au nguo nye pesi sana bila ya kusoma dua hasa nyakati za jo to 2.wakati wa kufanya tendo la ndoa na wanandoa kusahau kusoma dua wakati wa tendo{na hapa ndipo huwaingia watu zaidi} 3.kujitazama ktk kioo kwa muda mrefu bila ya kusoma dua na hasa kwa wanaopenda kujitazama waki wa uchi 4.kuogelea ukiwa uchi katika vyanzo vya maji bila ya dua {hii hupelekea kuingiwa hasa ...

TIBA YA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

ASALAMU ALAYKUM     katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya jiji la dar na ulimwengu kwa ujumla imekuwa ni jambo la kawaida kuona mara kwa mara uuzwaji wa zinazoitwa dawa za kuongeza nguvu za kiume            jambo ambaloz amani halikuwepo kwani watu waliweza kuwa na nguvu za kutosha kulimudu tendo la ndoa bila kuhitajia dawa yoyote ile leo imekuwa kama desturi kama hujui dawa ya nguvu za kiume wewe hutakuwa mganga na hutapata mtu wa kumtibu kwani ni zaidi ya asilimia 60% ya wtakao hitaji tiba watahitaji dawa ya nguvu za kiume jambo lililonipelekea kuandika makala hii ambayo nataraji itakuwa na manufaa kwa wengi  NGUVU ZA KIUME Ni hali ya mtu kuweza kumudu tendo la ndoa na kiasili hakuna ugonjwa wa nguvu za kiume bali kuna upungufu wa nguvu za kiume NINI CHANZO CHA TATIZO HILI kuna sababu nyingi znazopelekea upungufu wa nguvu za kiume miongoni mwazo ni; kuugua kwa mu...

FAIDA ZA KITUNGUU SWAUM

KITUNGUU THAUM (Swaumu/Saumu): Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni kitunguu swaumu. Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa. Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum . Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba. Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu. Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Warumi. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana. Kuna baadhi ya ...