NENDA MZEE ‘NGOSHA’ MUDA WAKO UMEFIKA LAKINI UMEACHA SOMO
Kutupwa na serikali kwa Mzee Ngosha (Francis Kanyasu) (86) aliyedaiwa kuchora Nembo ya Taifa ambae amefariki dunia karibuni kwenye matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ni kielelezo cha hali na maisha ya wazee ndani ya Tanzania na ulimwengu wote wa kidemokrasia, licha ya mchango wao mkubwa.
Ikiwa hiyo ndio hali ya mtu anaehisabiwa kutoa mchango muhimu kwa taifa. Vipi hali za wazee wengine hususan vijijini?
Licha ya unaohesabiwa mchango mkubwa alioutoa, Mzee Ngosha alikuwa fukara wa ‘kutupwa’ akiishi kwenye kijichumba kimoja Buguruni, Malapa kwa hisani ya mwenye nyumba na majirani. Ni baada ya vyombo vya habari kuibua taarifa zake ndipo serikali ikajitoa kimasomaso kumpeleka Hospitali kwenda kumalizika.
Demokrasia ni mfumo wa kinyama
Maoni